RAIS WA FIFA SEPP BLATTER AWAPONGEZA AZAM FC KWA KUTWAA UBINGWA WA LIGI KUU

Kikwete na Sepp BlatterNa Azam Fc

Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Sepp Blatter ametuma salamu za pongezi kwa mabingwa wapya wa Tanzania Bara, Azam FC.

Blatter ameandika barua hiyo kwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na kutoa pongezi hizo.
Amewapongeza benchi la ufundi pamoja na wachezaji kutokana na kuweka rekodi mpya ya bingwa tofauti.

Malinzi amethibitisha kupokea barua hiyo ya Blatter na kusema atawakabidhi Azam FC, kesho.

Aidha, Malinzi naye ametuma pongezi hizo za ubingwa kwa Azam FC.

“Tutawakabidhi barua huyo ya Blatter kutoka Fifa, lakini tunawapongeza kutokana na kutwaa ubingwa,” alisema Malinzi.

Pongezi za Blatter kwa Azam FC ni za kwanza kwa rais huyo wa fifa kwa klabu iliyotwaa ubingwa Tanzania

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s