AZAM FC YAKABIDHIWA KOMBE RASMI, YAILOWESHA BAO 1 – 0 JKT RUVU, MBEYA CITY YAICHAPA MGAMBO JKT KIMOJA

AzamKatika uwanja wa Azam Complex,  matajiri wa jiji la Dar es salaam ‘Azam Fc’  wanalambalamba leo wamecheza mchezo wao wa kukamilisha ratiba  dhidi ya maafande wa JKT Ruvu  na kujikuta wakipata tena ushindi kupitia goli lililofungwa kipindi cha pili na Brian  Omonyi na hatimaye kuandika historia nzuri ya kutofungwa mchezo hata moja tangu ligi  ianze na kukabidhiwa rasmi ubingwa wao na rais wa Shirikisho la kandanda Tanzania TFF  Jamal Malinzi.

Azam2Kwa upande wa Mbeya City yenyewe imehitimisha ligi kuu ya Vodacom  Tanzania bara kwa kuwapa ladha mashabiki wake baada ya kuwatungua maafande wa Mgambo JKT  kwa bao moja bila majibu kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Huku goli pekee la ushindi la Mbeya City likifungwa na Said Kitanga kunako dakika ya 75 baada ya  kuachia shuti kali tokea winga wa kulia  na kujaa wavuni, hadi mpira unamalizika Mbeya City ndio waliotoka kifua mbele  na kuvuna pointi tatu za mchezo huo.

Baada ya mchezo huo kumalizika, wachezaji wa Mbeya City pamoja na viongozi wao walivishwa medali zao za ushindi wa tatu, kazi ambayo imefanywa na  mkuu wa wilaya ya Mbeya Dk.Noman Sigara.

Kwenye dimba la Sheikh Amri mkoani Arusha, wameshuhudia maafande wa JKT Oljoro wenyewe wakiipa mkono wa kwa heri michuano ya ligi katika msimu ujao baada ya kwenda sare ya kufungana kwa bao moja kwa moja dhidi ya Mtibwa Sukari.

Kwa hali jinsi ilivyo kwa sasa ni wazi vilabu vya Rhino Rangers, JKT Oljoro na Ashanti United vimeporomoka daraja na nafasi zao msimu ujao wa ligi vitakaliwa  na Polisi Morogoro, Ndanda Fc toka mkoani Mtwara na Stendi united ya Shinyanga ambavyo vitaonekana vipya katika msimu uao wa ligi kuu Tanzania bara..

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s