WEZI WAMLIZA M-RAP VITU VYENYE THAMANI YA MILIONI 4.

M-RapWezi ni miongoni mwa watu wasio na  huruma hata kidogo, hasa  pale wanapokukuta  katika anga zao.  Zao la B-Hitz, rapa M-Rap na wenzake, wikiendi iliyopita walikumbwa na tukio la kustajabisha baada ya kuvamiwa na watu wanaozaniwa kuwa ni vibaka  na kupukutishwa  vitu vyenye thamani ya shilingi milioni nne za kiTanzania.

Akiongea kwa masikitiko makubwa  na Gossip Cop ‘Soudy Brown’,  Hitmaker huyo wa usiende Mbali alisema kwamba, mida ya saa moja jioni wakati akielekea kufanya shoo kwenye ukumbi wa Dar Live, waliamua kupaki usafiri wao kwenye fukwe zinazotazamana na hospitali matawi ya juu ya Agha Khan na kuanza kupigana picha kwa mtindo wa flashi na ndipo ikawa rahis kwa wezi hao waliojificha kwenye vichaka kuwaona na kuwafwata wakiwa na mapanga huku wakiwataka watoe kile walichonacho.

Aliendelea kuchezesha taya zake  kuwa, kutokana na wao kutokuwa na kitu chochote cha kujihami, iliwalazimu watoe kwa roho nyeupe mazagazaga yao ya bei chafu ikiwemo Simu tatu iPhone5s, HTC1, Blackberry,  waleti ya rafiki yake iliyokuwa na kiasi kama cha shilingi laki tatu, cheni, kadi za benki, visa pamoja na camera aina ya Canon na kuwaacha wakiwa weupe.

Baada ya tukio hilo, M-Rap na wenzake walikwenda kutoa taarifa katika kituo cha polisi na kisha kuelekea Dar Live Mbagala ambako alifanikiwa kupiga shoo licha ya kuwa na uchungu wa kuibiwa mali zake.

Blogu ya Larrybway91 inampa pole Rapa M-Rap na Rafiki zake waliokumbwa na janga hilo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s