FRENCH MONTANA AMEKUFA NA KUOZA KWA MDOGO WAKE KIM KARDASHIAN ‘KHLOE’.

Rapa wa Marekani mwenye asili ya Morocco, French Montana ambaye kwa sasa amekuwa akihusishwa kutoka  kimapenzi na mmoja kati ya familia ya Kardashian ‘Khloe Kardashian’  ambaye ni ndugu wa mwanamke mwenye mahusiano na Kanye West aitwae Kim Kardashian, ingawa kumekuwa na taarifa za rapa huyo kukanusha vikali uvumi ulioenea licha ya kuonekana wakiwa pamoja  maeneo mbalimbali ya kula bata.

French Montana & Khloe Kardashian1

French monatana akijikinga na kamera za mapaparazi wakati wa mtoko wa chakula cha jioni na mrembo Khloe

Awali Khloe Kardashian alikuwa ni mke halali wa mcheza kikapu Lamar Odom ambae alitengana nae huku chanzo kikitajwa kuwa ni mchepuko wa mwanaume huyo nje ya ndoa na matumizi yaliyokithiri  ya dawa za kulevya.

French Montana & Khloe

French Monatana na Khloe Kardashian katika klabu ya Arizona mida mibovu.

Katika kudhihirisha kuwa amekufa na kuoza kwa mrembo huyo Daraja la kwanza, French Montana hivi sasa amekuwa akisaka kwa udi na uvumba eneo kubwa ambalo lipatalo kama skwea 4800 katika ameneo ya Hollywood ambalo linaweza kupangishwa kwa kiasi cha  dola za kimarekani 29,000 kwa mwezi zaidi ya milioni 30 za kitanzania,  ili aweze kumpangishia mwanadada Khloe kardashian litakalokuwa na vyumba vinne vya kulala, mabafu manne, bwawa la kuogelea, sehemu ya michezo na mazagazaga mengine kibao ikiwemo Sauna.

French & KhloeWakati hayo yakiendelea, mwanamke ambaye alikuwa zilipendwa wa French Montana ‘Nadeen Kharbouch’  amesema kwamba katu Khloe asifikirie kuwa mambo yatakuwa yapo sawa, kwa sababu Montana si mzuri kama vile anavyozani.

French na mtoto wake Kruz

French Montana akiwa na mtoto wake wa kiume KRUZ mwenye umri wa miaka 4.

Aliendelea kufunguka akisema kwamba, kwa miaka kadhaa walikuwa pamoja kabla ya French Montana hajatoka, lakini mambo yalianza kwenda mrama  mwaka 2012 wakati rapa huyo wa ngoma ya ‘Watchu Call That’  alipoanza kuingia kwenye ulimwengu wa usupastaa na kujikuta akimsahau mtoto aliyezaa nae aitwae Kruz mwenye umri wa miaka 4.

Gari jipya la MjombaNadeen KharbouchPichani(Kushoto) ni Nadeen Kharbouch ambaye alikuwa mke wa Rapa French Montana.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s