RAPA ANDRE JOHNSON WA WU-TANG CLAN AFYEKA NYETI ZAKE.

christ-bearer-andre-johnson-rapper-cuts-penis-off-jumps-balcony-480x0Hii ndio Dunia, ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni. Rapa aliyepata umaarufu kupitia kundi la Wu-Tang Clan ‘Andre Johnson’  AKA Christ Bearer amenusurika kupoteza maisha baada  kuukata  uume wake kwa kisu na kisha  kujirusha   ghorofani.

Tukio hilo lilitokea Jumatano majira ya asubuhi katika jengo la North Hollywood,  huku taarifa za polisi zikidai kwamba,  licha ya kukata sehemu zake nyeti alipatwa na majeraha kadhaa mwilini mwake hali iliyopelekea  akimbizwe katika hospitali ya Sinai kwa kile kilichodaiwa ni jaribio la kutaka kujiua.

Kwa sasa Johnson anapatiwa matibabu hospitalini hapo ingawa bado haijaweza kufahamika sababu ya yeye kufanya kitendo hicho. Tukio hilo limetokea  ikiwa ni siku moja  kupita tangu video ya wimbo wake wa Ooooh! aliomshirikisha Rugged Mork kuwekwa katika mtandao wa YouTube.

Itazame Video ya wimbo wake iliyoachiwa YouTube siku moja kabla ya majanga kumkuta

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s