Katika kuonyesha kunogewa na mtindo mpya wa picha ‘SELFIE’. Rais wa marekani Barack Obama amemkaribisha makamu wake wa Rais ‘Joe Biden kwenye mtandao wa Instagram kwa staili ya kupiga picha ‘Selfie’ pamoja iliyowekwa kwenye akaunti rasmi ya kiongozi huyo ambayo ina wafuasi wapatao Laki 1 na ushee.
Rais Barack Obama na Makamu wake wa Rais Joe Biden wakitokelezea katika SELFIE.
”Found a friend to join my first selfie on Instagram. Thanks for following and stay tuned. –VP” aliandika Biden kwenye ukurasa wake wa Instagram, wakati Obama aliandika ”Welcome to Instagram, Mr. Vice President.” kupitia ukurasa wake wa Facebook.
Unaweza ukatazama picha nyingine zaidi za makamu huyo wa Rais alizokwisha kuziweka kwenye ukurasa wake tangu ajiunge rasmi na Insta Aprili 16 mwaka huu, akiwa tayari ameshapakia picha tano ndani ya kipindi cha siku 3 tu. Chezea insta wewe