BONDIA FRANCIS CHEKA AFICHUA SIRI ZA USHINDI WA MARA KWA MARA.

Francis ChekaBondia nambari moja kwa ubora na anayeshikilia mataji manne makubwa nchini,  Francis Cheka ameweka bayana siri ya mafanikio na ushindi  wa mara kwa mara pindi awapo ulingoni ambao humfanya aweze kuitangaza Tanzania  kimataifa zaidi kwa upande wa ndondi za kulipwa.

Akichezesha taya zake kwenye mahojiano na kituo cha utangazaji ‘Radio One’,  alisema siku zote  hujiamini kupanda ulingoni endapo akikaa chini ya siku 40 bila ya kukutana na mwanamke.

”Mapambano yangu yote nayocheza, siwezi kujiamini kukaa chini ya siku 40 bila kukutana na mwanamke ndio najiamini na kucheza ulingoni hata mashabiki wangu nakuwa na furaha nao, lakini kama nitafanya chini ya hapo huwa sijiamini”. Alisema  Cheka

Bondia huyo sugu anatarajia kupanda ulingoni hapo kesho katika ukumbi wa TPA Sabasaba kuvaana na bondia Gavad Zohrehvand kutoka nchini Iran huku Francis Miyeyusho akionyeshana kazi dhidi ya bondia toka Thailand ‘Sukkasem Kietyongyuth’ mwenye rekodi ya kucheza mapambano 13 bila   ya kupoteza hata pambano moja.

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s