HII NDIO ORODHA ILIYOTOLEWA NA FORBES YA WASANII WATANO WA HIP HOP MATAJIRI ZAIDI DUNIANI.

Wasanii 5 wa Hip Hop matajiri zaidi Duniani

PUFFY DADY, DR.DRE, JAY Z, BIRDMAN, 50 CENT

Jarida marufu Duniani la Forbes ambalo hutoa orodha ya watu matajiri zaidi Duniani kila mwaka, kwa mara nyingine tena  limetoa orodha ya wasanii  watano matajiri wanaofanya  muziki wa kufokafoka ‘Hip Hop’.

Katika orodha hiyo Sean Combs ei kei ei Puffy Daddy ndiye anaongoza katika orodha hiyo kwa kuwa msanii tajiri kwa mwaka huu.

Utajiri wake unakadiriwa kufikia kiasi cha dola za kimarekani milioni 700 ukiwa umeongezeka kiasi cha dola milioni 120  toka mwaka jana. Hiyo ni kutokana na televisheni yake ya REVOLT pamoja na mvinyo anaoutengeneza wa CIROC na kampuni zake nyingine kama vile BAD BOY ambavyo vimechangia kwa kiasi kikumbwa kumuweka kileleni.

Akifuatiwa na producer Andre Romelle Young AKA  DR.Dre akiwa na utajiri unaofikia dola milioni 550, huku utajiri wake ukitokana na mauzo ya Headphones zake za BEATS BY DRE sambamba na mziki anaozidi kuufanya.

Katika nafasi ya tatu anakaa mtu mzima Sean Carter ‘Jay Z’  au unaweza kumuita baba Blue Ivy akiwa na utajiri wa kiasi cha dola milioni 520 huku vyanzo vya utajiri huo vikitajwa kuwa ni kampuni yake ya mavazi ya Roca Wear, Live Nation pamoja na Roc Nation.

Wakati nafasi ya nne ikikamatwa na Bryan Adams al maarufu kama BIRDMAN huku utajiri wake ukitokana na  CASH MONEY, YMCMB na GTV Vodka akiwa na utajiri wa milioni 160.

Na aliyeshikilia nafasi ya tano ni Curtis Jackson maarufu kwa jina la jukwaani 50 Cent akiwa na utajiri wa milioni 140, vyanzo vya mapato yake vikitajwa kuwa ni maji yake anayoyauza ‘VITAMIN WATER’, SMS AUDIO Headphone na SK Energy

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s