KESI YA MWANARIADHA OSCAR PISTORIUS YAPIGWA KALENDA MPAKA MEI 5, AENDELEA KUJIUMAUMA

 Oscar Pistorious

Kesi ya Mwanariadha nyota wa mbio za paralyimpiki kutoka Afrika kusini, ‘Oscar Pistorious’ bado inaendelea kuunguruma  akikabiliwa   na kosa la mauaji ya kupanga kwa kumfayatulia risasi mara nne mfululizo aliyekuwa mpenzi wake Reeva SteenKemp yaliyotokea mwaka jana katika siku ya wapendanao

Oscar amemaliza kuhojiwa na jopo la wanasheria licha ya kuendelea kushikilia msimamo wake wa kuua bila kukusudia ingawa alishindwa kujibu  baadhi ya maswali ya papo kwa papo   hali iliyopelekea kuomba msaada kutoka kwa mwanasheria  wake.

Moja ya swali alilopigwa mwanamichezo huyo ni pale alipoulizwa kipindi anafyatua risasi, alihisi mpenzi wake yupo wapi??? Je,  hakuweza kusikia sauti ya mtu akilalamika baada kufyatua risasi ya kwanza ???? Hayo ni miongoni mwa maswali yaliyomtoa machozi Oscar.

kesi hiyo imehairishwa tena mpaka tarehe 5 Mei kwa ajili ya kupisha sikukuu za pasaka na endapo atapatikana na hatia staa huyo anaweza kukumbana na kifungo cha miaka 25 au akamalizia maisha yake gerezani.

 

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s