MAKAHAKAMA KUU NCHINI INDIA IMETHIBITISHA KUITAMBUA JINSIA YA TATU ‘TRANSGENDER’.

India yaitambua jinsia ya tatuMahakama kuu nchini India imeidhibitisha kuwatambua watu wanaobadili viungo vyao vya uzazi kama  jinsia ya tatu ‘Transgender’ na kupewa kibali cha kupatiwa huduma zote muhimu za kijamii ikiwemo elimu, afya, ajira pamoja na kuandikishwa katika daftari la kudumu la kupiga kura na hivyo kuwapa nafasi matabibu kuweza kuwasaidia watu watakaohitaji kubadili viungo vyao vya uzazi. Kwa sasa watu hao nchini humo wametambulika rasmi.

”Naipongeza mahakama kuu ya India na kwa mara ya kwanza leo najihisi  ni raia wa India. Naelewa tutakuwa na mabadiliko mengi maishani mwetu ingawa itachukua muda. Mahakama kuu imefungua mlango wa sheria lazima tusonge mbele kuanzia hapa”. Alisema mwanaharakati wa India.

”Naona ni kitu ambayo ingefanyika kitambo sana, lakini tusikuwe na matumaini kwamba hiyo ndiyo suluhisho pekee la kutatua watu wanaobadilisha jinsia”. Aliongezea mwanaharakati kutoka Kenya Odri Mbugua mtetezi wa  watu wanaobadili jinsia kwa kimombo ‘Transgender’  ambaye hapo awali alizaliwa na viungo vya uzazi vya kiume kabla ya kuamua kubadili jinsia yake..

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s