BONDIA MANNY PACQUIAO AMCHAPA TIMOTHY BRADLEY KWA POINTI.

Manny P

Bondia mfilipino ‘Manny Pacquiao’ amerejesha heshima yake baada ya  kumchapa bondia Timothy  Bradley wa Marekani katika mpambano uliodumu kwa dakika 36  kwenye ukumbi wa MGM Grand Garden Arena jijini Los Vegas hapo jana  . Pacquiao alitumia kasi na uzoefu aliokuwa nao kumshinda mpinzani wake Bradley ingawa haikuwa kazi ndogo kwani mpinzani wake huyo alikuwa akitupa makonde ya maana na kushambulia mwanzo mwisho.

Majaji wawili walitoa pointi 116 – 112 na wa tatu akatoa pointi 118 – 110 , na kumuwezesha Pacquiao kuibuka mbabe kwa jumla ya  pointi  199 – 109 katika pambano hilo. Awali mabondia hao walikutana kwa mara katika pambano walilocheza mwaka 2011, hali iliyopelekea Bradley kutoridhishwa na uamuzi uliotolewa na majaji waliompa ubingwa Manny na kuamua kurudiana nae.

Pambano hilo linamfanya mfilipino huyo kuingiza kibindoni kiasi kisichopungua  dola za kimarekani milioni 20(Tsh bilioni 32). Pacquiao atakuwa bondia wa pili kupata dola za kimarekani milioni 700 ambazo ni sawa na Tsh bilioni 1 na milioni 120 kwa malipo ya televisheni katika historia ya mchezo wa ngumi mwengine akiwa ni Floyd Maywheather ambao wote wamempiku Oscar de la hoya ambaye pambano lake na Tim Bradley  alilipwa dola za kimarekani  milioni 661 wakati Maywheather atapanda dau la dola milioni 756 atakapopambana na Marcos Maidana mwezi ujao.

Bondia Pacquiao tayari ameshaweka rekodi ya kuwa bondia pekee asiye mmarekani kuingia katika orodha ya tano bora ya mabondia wanaolipwa malipo mazuri ya haki za televisheni ambayo Evander Hollyfield  na Mike IRON Tyson wanashika nafasi ya nne na ya tano nyuma ya De La Hoya.

 

Manny Pac  Pacquiao akimsulubu kwa makonde mazito mpinzani wake Tim BradleyManny Pacquiao

Kipigo kilipokolea.

Manny Pacquiao1

Bradley akikwepa konde zito mithili ya nyoka kutoka kwa Manny.

Manny1Hapa ni wakati Pacquaio alipotangazwa mbabe na mshindi wa pambano hilo.

Manny Pac2Mama mzazi wa bondia Manny Pacquiao alishindwa kuzuia hisia zake, kama anavyoonekana akiwa amebeba glovu alizotumia mwanae kumchapa Bradley.

Tazama video ya mpambano huo hapo chini.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s