PICHA : SHETTA APATA AJALI MBAYA AKIWA NJIANI KUELEKEA BABATI.

Mwanamuziki wa Bongo fleva ‘Shetta’ ei kei ei baba Qayllah  amenusurika ajali mbaya alipokuwa njiani akielekea Babati mkoani Manyara kwa  ajili ya ziara yake ya muziki  ‘Kerewa Tour’ iliyokuwa ifanyike jana usiku.

Shetta anusurika ajaliniArusha 1#babati leo ndo siku yenu ile #kerewatour ofcoz mi ndo baba Qayllah… sikiliza mi sirudi nyuma alafu kushoto na kulia hakuna deal kama vipi we #angaliambeleeee. Picha na ujumbe Alioandika Shetta kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Arusha akitokea Dar kabla ya ajali kutokea.

Kwa mujibu wa taarifa zinasema kwamba, staa huyo wa ‘Nidanganye’ alipofika jijini Arusha akitokea Dar, alipokelewa na wenyeji wake na kisha safari kuanza kuelekea Babati.

Ripoti iliongeza kuwa, walipofika eneo moja lenye mbuga, ghafla  alikatisha pundamilia hali iliyopelekea  gari alilopanda msanii huyo kupinduka mara tatu kutokana na dereva wa gari hilo kufunga breki kwa minajili ya kumkwepa mnyama huyo.

nashukuru mungu nimetoka salama kweli mungu mkubwa mana nilijua leo ndo mwisho wangu mana ajali ni mbayaaa sanaaaaa...... thnx woteee mlionipa pole tupo pa1.Picha ni gari aina ya Toyota Noah alilokuwemo Shetta baada ya kuanguka mara tatu.

 ”nashukuru mungu nimetoka salama kweli mungu mkubwa mana nilijua leo ndo mwisho wangu mana ajali ni mbayaaa sanaaaaa…… thnx woteee mlionipa pole tupo pa1” aliandika Shetta.

Blogu ya Larrybway91 inampa pole  mwanamuziki Shetta na kumtakia   afya njema.

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s