BEYONCE, TIMBERLAKE NA PHARRELL WAONGOZA KUWANIA TUZO ZA BILLIBOARD.

Queen Bey

Mchakato tayari umeshaanza wa kutangazwa  majina ya wasanii watakaowania tuzo za Billiboard ambazo hufanyika kila mwaka. Wasanii kama vile Justin Timberlake, Beyonce Knowles na Pharrell Williams wameongoza kutajwa katika vinyanganyiro hivyo  kushinda wanamuziki wengine.

Beyonce ndiye anashikilia usukani kwa upande wa wanawake akitajwa kuwania  vipengele 7 ikiwemo cha mwimbaji bora wa kike wa R&B, albamu bora ya Billboard na albamu bora ya R&B, wakati kwa wanaume Justin Timberlake  ameongoza kwa kutajwa  kuwania tuzo hizo katika vipengele 11 kupitia albamu yake (20/20 Experience) ikiwemo tuzo ya msanii bora, wasanii 100 bora na muimbaji bora wa kiume wa R&B.

Akifuatiwa  na Pharrell Williams aliyetajwa kuwania  vipengele 7 ikiwemo kolabo ya wimbo wa ‘Blurred Lines’  alioshirikishwa na Robin Thicke pamoja na Rapa  T.I  ambao nao pia wametajwa kushindania vipengele  5.  Rihanna  naye hakuachwa nyuma bali ameteuliwa kuwania vipengele 5 wakati baba yao ‘Jay Z’ akitajwa  katika vipengele vikubwa 4 kupitia albamu yake mpya ya ‘Magna Carta Holly Grail’ na kibao  alichoshirikiana na mkewe ‘Queen Bey’ kinachoitwa ”drunk in love”.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s