RIDHIWANI KIKWETE ASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE CHALINZE.

Ridhiwani1Ridhiwani Kikwete akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura mjini Chalinze jana.

Na kikosi kazi cha FullShangwe Chalinze

Ridhiwani Kikwete aliyekuwa mgombea ubunge uchaguzi mdogo jimbo la Chalinze Bagamoyo mkoani Pwani kupitia Chama cha Mapinduzi CCM ameibuka kidedea kwa asilimia 86.61 katika uchaguzi huo na kuwamwaga wagombea wengine kutoka vyama vinne vya upinzani.

Matokeo ya uchaguzi huo yanaonyesha Ridhiwani ameongoza akifuatiwa na CHADEMA ,CUF,NRA na ASP.

Matokeo hayo yametangazwa usiku wa kuamkia leo April 7 majira ya saa nane usiku katika shule ya sekondari Chalinze na  Msimamizi wa uchaguzi huo  Bw.Samwel Salianga ambapo amesema CCM –Ridhiwani Kikwete amepata kura  20,828 sawa na  86.61%,Chadema-Mathayo Torongei amepata kura 2,544 sawa na asilimia 10.58,CUF- Fabian Skauki  476 sawa na asilimia 1.98,NRA-Hussein Ramadhani kura 60 asilimia 0.25 huku AFP Ramadhani Mgaya amepata kura 186 sawa na asilimia 0.59

Salianga amesema kati ya watu waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ni watu elfu 92,  waliojitokeza katika zoezi hilo ni watu 24,422 ambapo kura halali zilikuwa 24,047 na  kura 375 zikiharibika.

Wagombea waliokuwepo wakati wa kutangaza  matokeo katika uchaguzi huo na kusaini fomu ya kukubalina na matokea alikuwepo mgombea wa NRA na CCM pekee.

Aidha Wakizungumza baada ya kupokea matokeo hayo aliyekuwa mgombea wa chama cha NRA pamoja na Ridhiwani Kikwete kupitia CCM,kila Mmoja ameshukuru wananchi na kuahidi kushirikina na wananchalinze kuleta maendeleo.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s