THE GAME KIZUIZINI KWA KUMPA KIPONDO MCHUMBA WAKE.

RAPA mtukutu mzaliwa wa  Compton, Marekani kwa jina  ‘The Game’ amejikuta akiwa chini ya uchunguzi  kufuatia   mchumba wake Tiffney Cambridge kumfungulia mashtaka polisi kwa madai ya kumshambulia na kumjeruhi vibaya maeneo ya  usoni, sikioni  na puani.

The GameThe game aliyeegemea ukuta akiwa na rafiki yake ‘The Money Gang WorldWide’ kabla ya kupelekwa kwenye mahojiano na maafisa wa Sherriff .

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ ulidai The Game alibadili hali ya hewa na kumshambulia Tiffney wakati wakiwa kwenye mazungumzo.

”Game anatuhumiwa kwa kosa la unyanyasaji ..baada ya kudaiwa kumpiga mchumba wake, ilisema sehemu ya taarifa kutoka kitengo cha ‘L.A Sherriff’ ambacho kinafanyia uchunguzi tukio hilo.

”Sitaka kuelezea sana shutuma hizo  za uongo, lakini ukweli utakuja kujulikana. Mimi daima naangalia usalama wa mtoto wangu na sijawahi kumpiga Tiffney. alisema  The Game akikanusha madai hayo kuwa sio ya kweli.

Aliongezea kwa kuweka picha inayoonekana hapo chini kwenye ukurasa wake wa Instagram iliyokuwa ikipinga madai yaliyotolewa…

Txt

Muda mfupi baadae Tiffney alirudisha majibu kupitia mtandao huo akiendelea  kushikilia msimamo wake wa kupigwa na kudai rapa huyo wa kibao cha ‘Jesus Piece’  ni muongo.

Game na Tiffney wamedumu katika mahusiano kwa kipindi kirefu  mpaka kufikia hatua ya kuangaza maisha yao kupitia kipindi cha ‘Marring The Game’  kinachorushwa na  VH1 ingawa siku za hivi karibu kumetokea hali ya kutoelewana baina yao jambo linalohatarisha  malezi bora kwa mtoto wao wa kike ‘Cali’. 

The Game Daughter mtoto wa The Game aliyezaa na Tiffney anayeitwa ‘Cali’.

 

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s