HOTELI YA PICCOLO BEACH YATEKETEA KWA MOTO JIJI DAR ES SALAAM.

 

Image

Image

Image

Hotel ya Piccolo (pichani) iliyoko jijini Dar es Salaam pembezoni mwa ufukwe wa bahari ya Hindi katika eneo la Kawe, leo majira ya saa nane iliwaka moto eneo la restaurant na kusababisha vitu kadhaa kuteketea.

 

Kwa mujibu wa mmoja wa wafanyakazi wa Piccolo aliyetoa maelezo na kutotaka jina lake kutajwa alieleza kuwa moto huo ulisababishwa na hitilafu ya waya za umeme, ambapo cheche ziliangukia nyasi zilizoko katika paa la restauranti hiyo na kushika moto kwa kasi.

“Moto ulianza ghafla na kusambaa hivyo ukuanza kushika paa la restaurant, tulijitahidi kuzima na kufanikiwa hata faya walipofika tulikuwa tumesha maliza” alieleza dada huyo.

Baada ya moto kushika kasi, wafanyakazi kwa umoja wao walianza kuuzima kwa kutumia maji yakiwemo ya bwawa la maji la kuogelea (swimming pool). Kutokana na umoja wa wafanakazi hao walijitahidi kuzima moto huo.

Kampuni inayolinda hoteli hiyo ya Kiwango Security, waliita gari la zimamoto la shirika la Knight Support lililokuwa mbali mpaka kufika eneo la tukio tayari shughuli kubwa ilikuwa imeshafanywa na wafanyakazi wa hoteli hiyo.

Hasara iliyosababishwa na moto huo haikuweza kufahamika maramoja, japokuwa walioshuhudia wanasema waliweza kuudhibiti moto huo kiasi haukufika maeneo mengine yaliyoko karibu na restauranti kama jikoni, vyumbani, kumbi za mikutano na harusi, baa na maeneo mengine.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s