afande sele

AFANDE SELE ATANGAZA NIA YA KUWANIA UBUNGE MOROGORO

Mwanamuziki wa kizazi kipya, Suleimani Msindi ‘Afande sele’, ametangaza nia ya kuwania ubunge wa Morogoro mjini kupitia Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania). Msanii huyo ametangaza azma yake baada ya kujiunga na chama hicho akitokea Chama cha Chadema akifuata nyayo za Mheshimiwa Zitto Kabwe.  Nini ungependa kumshauri Afande Sele? Chanzo : EATV

Polisi

WAGANGA WA KIENYEJI WAWACHIMBA MKWARA POLISI

Wakati msako wa kuwakamata waganga wapiga ramli chonganishi ukiendelea nchi nzima hasa katika mikoa ya kanda ziwa, jeshi la polisi nchini limepewa onyo toka kwa wanganga wa jadi juu ya vifaa vinavyokamatwa wakati wa msako wao. Jeshi hilo limepewa tahadhali ya kukumbana na hatari yeyote baadaye ikiwa wataendelea kukamata vifaa hivyo vikiwamo vibuyu, vitambaa vyeupe…

Madonna X Jay Z

MAKUBWAAAA!!! MADONNA ATAKA KUWA MKE WA PILI WA JAY Z

Malkia wa muziki wa pop Dunia, Lady Madonna, amesema anatamani kupata nafasi ya kuwa mke wa pili wa rapa Jay Z. Madonna ameyasema hayo baada ya kuona kila mialiko anayotoa Rais Obama imekuwa ikimpita pembeni na hivyo kulazimika kusema wazi kuwa labda angeolewa na Jay Z angeweza kupata mwaliko. ”Miongoni mwa watu naotaka kukutana nao…

kim-kylie-tyga-blac-chyna

KYLIE JENNER AMTAMBIA BLAC CHYNA MTANDAONI

Mdogo wa kufukia wa Kim Kardashian, Kylie Jenner, anadaiwa kumtambia ex na baby mama wa Rapa Tyga, Blac Chyna, kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram. Ishu hiyo inatajwa kutokea usiku wa jumanne(Mar.24) baada ya Chyna ku-post picha Instagram  akiwa ametupia saa ya bei mbaya inayosemekana alinunuliwa na Tyga enzi za mapenzi motomoto.  Hata hivyo haikupita…

Shikorobo Flyer

KICHUPA KIPYA : SHETTA FEAT. KCEE – SHIKOROBO [Official Video]

Hitmaker wa Kerewa, Shetta, ameonyesha kufuata nyayo za swahiba wake, Diamond Platnumz, baada ya kuachia video kali mpya ya ngoma yake ‘Shikorobo’ akiwa amemshirkisha mwanamuziki nyota wa nigeria ‘Kcee’ ambayo imefanywa nchini Afrika Kusini na kampuni ya Godfather Productions.  Itupie jicho Hapo chini kwa mara ya kwanza  

Baucha

BAUCHA AMUANIKA BINTI YAKE, SHE’S SO CUTE

Hitmaker wa Champododo, Titto Baucha, amewaonyesha mashabiki wake kuwa amekwisha kula magunia mengi ya chumvi baada ya kutokelezea katika picha ya pamoja na binti yake mkubwa aitwaye Natacia. Mmiliki huyo wa studio za Baucha Records aliandika, ”Baucha,Natacia” na  kuwapa nafasi fans wake kucomment katika picha hiyo aliyopost katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa…

Zitto Kabwe

ZITTO KABWE ATANGAZA RASMI KUACHIA UBUNGE

Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini kupitia tiketi ya CHADEMA, Zitto Zuberi Kabwe, amewaaga rasmi wabunge wa jamhuri ya muungano wa Tanzania jioni ya leo mara baada ya kumalizika kwa shughuli za Bunge. Aidha Mbunge huyo ametangaza rasmi kuachia nafasi ya ubunge wa jimbo hilo kufuatia mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, kutangaza katika vyombo…

Jose chameleone X Ak47

JOSE CHAMELEONE AFIWA NA MDOGO WAKE

Mwanamuziki nyota wa Uganda, Jose Chameleone, amepatwa na pigo kubwa la kuondokewa na mdogo wake wa damu ‘Emmanuel Mayanja’ maarufu kama Ak47 ambaye pia ni mwanamuziki wa miondoko ya dancehall nchini humo. Kifo cha Ak47 kimeripotiwa kutokea ghafla baada ya kuanguka bafuni katika pub moja inayoitwa Dejavu iliyopo eneo la Kansaga Jumatatu usiku(Mar.16) kabla ya…

Cheka

BONDIA FRANCIS CHEKA ABADILISHIWA KIFUNGO

Hukumu ya Cheka ambayo imebadilika kutoka miaka 3 hadi miaka miwili kulingana na sheria namba 6 ya mwaka 2002 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2004 imemtaka mfungwa kufanya kazi masaa 4 bila malipo katika taasisi za umma. Sheria hiyo imemuwezesha bondia huyo kutumikia kifungo chake cha nje ambapo atatakiwa kufanya kazi katika taasisi za umma ikiwemo kwenye…

linex X Diamond - Salima

KICHUPA KIPYA : LINEX Feat. DIAMOND PLATNUMZ – SALIMA [Official Video]

Linex ameitendea haki kauli ya bandika bandua kufuatia kuwapa ladha mashabiki kupitia ngoma yake ya Salima akiwa amemshirkisha Diamond ambayo aliyoiachia siku chache zilizopita na kama hiyo haitoshi msanii huyo ameendelea kuwapa ladha fans wake kwa kuachia kichupa cha single hiyo ambacho kimeongozwa na dairekta Adam Juma wa Next Level.  Itazame hapa kwa mara ya…

Diamond Platnumz

DIAMOND AFANYIWA UPASUAJI WA MGUU

Mfalme wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, amefanyiwa upasuaji mdogo kwenye mguu wake wa kushoto katika hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni jijini Dar es salaam. Diamond ameiambia Blogu ya Larrybway91 kuwa upasuaji huo ulichukua saa kadhaa ambao ulihusisha utolewaji wa kitu chenye asili ya chupa kilichokuwa kimekaa mguuni mwake kwa takribani mwaka mzima. ”Nilikuwa na kichupa…