Psquare Naija

ZITUPIE JICHO PICHA 14 MPYA ZA PSQUARE

Mapacha wawili, Peter na Paul Okoye wanaounda kundi la Psquare wameachia picha kali  kwa ajili ya promo ya ujio mpya wa albamu yao ya sita inayotarajiwa kuingia rasmi sokoni mwezi September mwaka huu. Baadhi ya picha hizo wakali hao wanaonekana wakiwa wametupia clothing line ya kaka yao Tony Okoye  ”Ajeh wears” ambazo zimekuwa gumzo hasa…

mYMABA

PASTOR MYAMBA APATA AJALI YA GARI

Staa wa Bongo Movie, Pastor Myamba amepata ajali  ya gari baada ya mkoko wake kugongana ubavuni na gari lingine ikiwa ni wiki kadhaa kupita tangu afunge ndoa takatifu na mkewe Praxceda visiwani Zanzibar. Hata hivyo ajali hiyo haikuweza kumletea madhara yoyote msanii huyo anayezitendea haki scene za kichungaji na kuandika kwenye ukurasa wake wa Facebook…

Big sean na Ariana Grande

MCHUCHU MPYA WA BIG SEAN AGOMA KUMWAGA MCHELE KWENYE KUKU WENGI

Kinda wa miondoko ya R&B kutoka majuu, Ariana Grande amegoma kabisa  kumwaga mchele kwenye kuku wengi juu ya kile kinachoendelea kati yake na Rapa Big Sean wakati alipofanyiwa mahojiano na mtangazaji maarufu Ryan kwenye Ryan Seacrest Radio Show. Ariana mwenye umri wa miaka 21  alijikuta akimung’unya maneno baada ya kuulizwa kama yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na Big sean ambaye  awali…

Straika wa Milton Keynes Dons, Will Grigg akishangilia baada ya kutikisa nyavu za United

AIBU NYINGINE!!! KEYNES DONS YAICHAKAZA 4 – 0 MAN UNITED

  Matokeo mabaya yameendelea kuwatafuna Mashetani wekundu baada ya kukubali kipigo cha aibu cha mabao 4 – 0 kutoka kwa Milton Keynes Dons hapo jana(Agosti26) katika michuano ya kuwania kombe la Capital One. Mtanange huo ulionekana kuwaelemea United chini ya kocha mkuu Louis Van Gaal na kujikuta wakiruhusu mvua  ya magoli langoni mwao kupitia William…

Di Maria na Van Gaal

ANGEL DI MARIA ATUA OLD TRAFFORD

Kiungo  wa kimataifa wa Argentina, Angel Di Maria ametia saini mkataba wa miaka mitano kukitumikia kikosi cha mashetani wekundu klabu ya Manchester United kwa ada ya uhamisho wa pauni  milioni 59.7 akitokea Real Madrid ya Hispania. Di Maria mwenye umri wa miaka 26 anakuwa mchezaji wa pili wa United kulipwa mshahara mnono zaidi akiwa nyuma ya…

Nigeria

SHULE ZAFUNGWA NIGERIA KWA HOFU YA EBOLA

Shule zote nchini Nigeria zilizokuwa zianze muhula mpya jumatatu zimeagizwa kuahirisha siku ya kufungua muhula hadi oktoba tarehe 13 kama moja wapo ya njia za kuzuia kuenea kwa viusi vya Ebola. Waziri wa elimu Ibrahim Shekarau ameamuru zisifunguliwe ili kuwapa walimu mafunzo jinsi ya kushughulikia ugonjwa huo. Inatarajiwa angalau wafanyakazi wawili kila shule katika zile…

Mario Balotelli

LIVERPOOL YAKAMILISHA USAJILI WA BALOTELLI, APEWA JEZI NAMBARI 45

Majogoo wa jiji la London, Liverpool wametangaza rasmi kukamilisha taratibu za kumsajili mpachika mabao mtukutu ‘Mario Balotelli kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 16 akitokea Ac Milan ya Italia. Balotelli ameichezea  Milan  kwa takribani mwaka mmoja na nusu akiwa amekwishaifungia mabao 30 katika michezo 54 aliyocheza. ”Nina furaha. Tumekuwa tukiongea kuhusu kuja hapa na…

J.Lo na Casper Smart

KUNANI TENA, JENNIFER LOPEZ NA SERENGETI BOY WAKE???

Kama waswahili wasemavyo, ” Penzi kiti cha basi, ukishuka wanakaa wengine” lakini msemo huo umeonekana kutomwingia akilini mwanamama na mwanamuziki Jennifer Lopez baada ya kufumwa na kamera za CCTV usiku wa Jumapili(agosti24) wakati utoaji wa Tuzo za MTV VMA akiwa beneti na serengeti boy wake Casper Smart ambaye alimpiga chini miezi kadhaa iliyopita. Casper Smart…

Stevan Jovetic

MAN CITY YAIFUMUA 3 – 1 LIVERPOOL

Kocha mkuu wa manchester City, Manuel Pellegrini hataki mchezo kabisa hasa linapokuja suala zima la kugombea pointi tatu muhimu katika msimu huu mpya wa ligi kuu ya England  baada ya kuwaangushia kichapo cha bao 3 – 1 majogoo wa jiji la London ‘Liverpool’ katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la  Etihad usiku wa jana. City ndio…

2face Idibia

2FACE IDIBIA AFIWA NA BABA YAKE MZAZI

Hitmaker wa african Queen, 2Face idibia amepatwa na msiba mzito wa kumpoteza baba yake mzazi Mzee Michael Agbo Idibia aliyefariki Dunia Jumamosi ya Agosti 23 katika hospitali moja mjini Abuja nchini Nigeria baada ya kusumbuliwa kwa kipindi kirefu na saratani ya tezi dume maarufu kama Prostate Cancer. Marehemu Idibia amezaliwa Julai 25 mwaka 1946 na…